Vitendo vya unyanyasaji wa mabinti wa kazi majumbani vimeendelea
kuripotiwa jijini Dar es Salaam baada ya binti mwingine Melina Mathayo
mwenye umri wa miaka 16 kukatwa katwa sehemu ya kichwa na kung'atwa
ikiwa ni adhabu aliyokuwa akipewa kwa zaidi ya miaka miwili na mwajiri
wake Yasinta Chengula huko Boko.