MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo, Ali Choki
amepata pigo la kuondokewa na mke wake, Shuea Hamis ‘Mama Shuu’ baada ya
kuugua kwa muda mrefu Usiku wa kuamkia leo.
Akizungumza kwa masikitiko Ali Choki alisema mke wake ameugua kwa
muda wa miezi tisa akiwa anasumbuliwa na mguu ambapo alitibiwa nchini
India ikashindikana akarudishwa nyumbani mpaka mauti yalipomfika usiku
wa kuamkia Jumamosi iliyopita.
“Ukweli nimeumia kwani mke wangu ndiye aliyekuwa mshauri wangu mkuu
na ndiye kila kitu kwangu alikuwa akinisapoti kwenye kazi yangu ya
muziki lakini ndiyo hivyo Mungu amempenda zaidi sina la kufanya,”alisema
Ali Choki.
Aidha Choki alisema mipango ya mazishi ilifanyika nyumbani kwao
Tuangoma Kigamboni na mazishi ya mkewe yalifanyika jana saa
kumi jioni katika makaburi ya Chang’ombe Madukamawili.
(Habari na Gladness Mallya/GPL)