Tamasha la Upendo kwa mama litafanyika tena kwa mara ya pili ndani ya jiji la Arusha kutokana na kuvunjika kwa tamasha la awali kutokana na mvua kubwa kunyesha katika mkoa huo siku ya juma pili ya Tarehe 02Nov 2014.
Kutoka na Tamasha hilo kushindwa kuendelea Kampuni iliyohusika na uandaaji wa Tamasha hilo ya MKUNDI PRODUCTION,Imeamua kuwarithisha mashabiki wa nyimbo za Injili hapa Tanzania na nje ya nchi kwa kurudia tena Tamasha hilo buer bila kiingilio.
Tamasha hilo litafanyika siku ya tarehe 16 Nov 2014 Katika uwanja wa Shekh Amri Abed Karume kama ratiba ya awali ilivyokuwa ikijieleza.
Waimbaji ambao watahudumu siku hiyo ni pamoja na Upendo Nkone,Martha Mwaipaja,Christina Shusho,Rebbeca Magaba,Eng Carlos Mkundi,Massa Baraka pamoja na wasanii kutoka sehemu mbalimbali nchini.
Sambamba na hayo pia MKUNDI PRODUCTION Imeaandaa tamasha lingine ambalo litafanyika ndani ya Mji wa Moshi tare 30 Nov 2014,katika kiwanja cha Ushirika Moshi MUCCOBS kwa kiingilio cha shilingi 3000/kawaida pamoja na shl 10000/=kwa VIP Ambapo watakuwepo waimbaji lukuki ambao wameongezeka kuja kuwapa burudani wakazi wote wa Moshi.