skip to main |
skip to sidebar
RIPOTI YA TAKUKURU YAZIDI KUCHAFUA HALI YA HEWA BUNGENI
Naibu Spika,Job Ndugai akiwaonya waabunge wa Upinzani bun geni jana kabla ya kutokea mtafaruku. Picha na fidelis Felix
Dodoma.
Sakata la uchotaji wa Dola za Marekani 200 milioni katika akaunti ya
Tegeta Escrow limeendelea kuibuka kwa sura mbalimbali bungeni. Safari
hii, Bunge limetakiwa kueleza ni kwa nini Ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) isifikishwe katika chombo hicho cha
kutunga sheria sambamba na ile ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG).
Hayo yalijitokeza bungeni jana baada ya
wabunge kadhaa kusimamia wakitaka mwongozo wa Spika kuhusu uchunguzi
huo, hasa kutokana na kuwapo taarifa kuwa ripoti ya CAG itawasilishwa
bungeni mwishoni mwa mwezi huu, lakini ile ya Takukuru ambayo pia
inachunguza suala hilo, haitapelekwa bungeni wala kujadiliwa.
Uchunguzi
wa Akaunti ya Escrow uliamuliwa na Serikali baada ya Mbunge wa Kigoma
Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila kulipua ufisadi uliotokana na
utata katika uchotaji wa fedha kwenye akaunti hiyo katika Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) baada ya kutokea mgogoro wa kibiashara baina ya Shirika
la Umeme Tanzania (Tanesco) na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL.
Katika
mgogoro huo, Tanesco ilikuwa inabishia kiwango cha fedha ilichokuwa
inalipa kwa gharama za uwekezaji kwa IPTL, ndipo ikaamuliwa na Mahakama
ifunguliwe akaunti hiyo ili fedha ilizokuwa inalipa ziendelee kuwekwa
huko hadi mgogoro utakapokwisha. Kesi hiyo iliamuliwa katika mazingira
yanayoelezwa kuwa na utata na fedha hizo kuchukuliwa haraka na IPTL.
Jana,
baada ya kipindi cha maswali na majibu, wabunge kadhaa walisimama wengi
wakiwa wa upinzani wakitaka mwongozo kuhusu lini ripoti hizo mbili
zitawasilishwa bungeni hasa baada ya ile ya Takukuru kuelezwa na
Mkurugenzi Mkuu wake, Dk Edward Hoseah kuwa imekamilika na kukabidhiwa
kwa Waziri Mkuu.
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema),
Joshua Nassari ndiye aliyefungua mlango wa kuomba mwongozo wa Spika
akitaka kujua ni lini ripoti hiyo itawasilishwa na kwa nini isiambatane
na ile ya CAG kwa kuwa zote zinatokana na maazimio ya Bunge kutaka
uchunguzi huo ufanyike.
Pia Nassari alihoji kwa nini mjadala wa ripoti ya CAG umepangwa siku mbili za mwisho kabla ya kumalizika kwa mkutano wa Bunge.
“Naomba maelezo kwa nini hii ya Takukuru haitaletwa wakati imeelezwa kuwa Waziri Mkuu ameshakabidhiwa?” alihoji Nassari.
Akijibu,
Naibu Spika, Job Ndugai alisema Kamati ya Uongozi imeshajadili suala
hilo na kuamua kwamba ripoti ya CAG itapitia kwenye Kamati ya PAC
inayoongozwa na Zitto Kabwe na kuwasilishwa bungeni.
“Ripoti
ya CAG itawasilishwa kwenye Kamati ya PAC na wabunge mtakabidhiwa
nakala kama tulivyokubaliana kwenye Kamati ya Uongozi,” alisema Ndugai
na kuongeza:
“Ripoti itawasilishwa tarehe 26 mwezi huu kama
ilivyorekebishwa kwenye ratiba. Kuhusu suala la kupangwa mwishoni ni
suala la kanuni kwa kuwa huwa tunaanza na shughuli za Serikali kwanza
halafu ripoti zinafuata.”
Kuhusu ripoti ya Takukuru, Ndugai
alisema haiwezi kuwasilishwa bungeni kwa kuwa taasisi hiyo ikishamaliza
shughuli zake inaweza kuchukua hatua kwa kupeleka taarifa kwa Mkurugenzi
wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya hatua zaidi.