global

global

Pages

Tuesday, June 3, 2014

MTOTO NASRA ALIYEISHI KATIKA BOKSI MIAKA MINNE SASA KUZIKWA LEO MAKABURI YA KOLLA BAADA YA WANANCHI KUAGA MWILI WAKE JAMHURI MANISPAA YA MOROGORO.

Jeneza lenye mwili wa mtoto Nasra Rashid (4) likishushwa kutoka kwenye gari ili kuingiza katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa wa Morogoro Hospitali ya Taifa ya Muhimbi jijini Dar es Salaam. Picha na Juma Mtanda.

Dar es Salaam. 

Ndugu wa baba wa mtoto, Nasra Mvungi (4) aliyefariki dunia usiku wa kuamkia juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jana walijitokeza wakitaka wapewe mwili wa marehemu kwa ajili ya maziko.

Baada ya kuwasili hospitalini hapo saa 1:35 asubuhi, ndugu hao wakiongozwa na baba wa mtoto huyo, Rashid Mvungi walikutana na maofisa wa ustawi wa jamii wakiongozwa na Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungatuti wakitaka wakamzike mtoto wao kwa kufuata imani ya dini yao ya Kiislamu.

Hata hivyo, Ngungatuti alipinga hoja hiyo akisema suala la ndugu kuzika halina nafasi na kwamba mtoto atazikwa na ustawi wa jamii ambao ndiyo waliokabidhiwa mtoto huyo na polisi.

“Tutamzika kiserikali kwa kuzingatia imani ya dini yake lakini hatutawakabidhi maiti kwa namna yoyote,” Ngungatuti alisema na kuongeza kuwa wanafanya hivyo kwa kufuata misingi ya kisheria.

Akizungumzia suala hilo Mvungi alisema: “Ndugu zangu wanataka mtoto tupewe lakini kama sheria inakataza mimi sina neno ila kama ingekuwa ni matakwa yangu ningependa nipewe mwanangu nikazike mwenyewe.

Sakata hilo liliendelea mjini Morogoro ambako baada ya mwili kuwasili, watu wanne; wanawake wawili na wanaume walifika Ofisi za Ustawi wa Jamii na kujitambulisha kuwa ni bibi na wajomba wa marehemu wakitaka wapewe mwili wa mtoto huyo.

Hata hivyo, Ofisa Ustawi wa Jamii mkoani Morogoro, Yolanda Mkapa aliwataka waende polisi kupata kibali kabla ya kupewa mwili huo. Baada ya majibu hayo, walitazamana na kuamua kuondoka huku wakiacha maagizo kuwa washirikishwe katika mchakato mzima wa maziko.

Akizungumzia hali hiyo, Ngungatuti alisema hofu ya wanandugu pengine ni kudhani kuwa rambirambi na misaada mingine itakayotolewa itatumika visivyo dhana aliyosema si sahihi kwani marehemu kabla ya kufikishwa Muhimbili alifunguliwa akaunti.

“Bahati mbaya amefariki na kutokana na hali hiyo fedha ambazo zitapatikana zitaendelea kutunzwa katika akaunti hiyo na zitawasaidia wenzake wengine wenye matatizo kama yeye wanaopokewa na idara.”

Akizungumzia msiba huo, mlezi wa mtoto huyo, Josephine Joel alisema amepata uchungu kwani aliamini kuwa Nasra angerejea hali ya kawaida akisema kabla hajafariki alihangaika sana.

Historia ya Nasra
Nasra aligundulika akiwa amefichwa katika boksi na mama yake mkubwa, Mariam Said huko Uwanja wa Ndege, Morogoro ikielezwa kuwa alikuwa humo tangu akiwa na umri wa miezi tisa alipomchukua kumlea baada ya mdogo wake (Mama Nasra), kufariki dunia