Polisi
nchini India wanasema kuwa kikundi cha madaktari kimempiga hadi kufa
mshukiwa wa wizi katika taasisi ya mafunzo ya udaktari mjini Calcutta
mashariki mwa India.
Mwanamume huyo alifungwa kwenye mlingoti na kucharazwa viboko huku uume wake ukikatwakatwa kwa wembe.
Polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo alidaiwa kuiba simu za mkononi.
Watu wawili wamezuiliwa na polisi huku uchunguzi ukiendelea kufanywa.
Wandishi wa habari wanasema kuwa mauaji hayo ni dalili ya tatizo la watu kuwaadhibu washukiwa wa uhalifu nchini India hadharani.
Lakini kinachoshangaza sana katika tukio hili ni kuhusika kwa madaktari katika kitendo hicho.
Madaktari
hao walimburuza mwanamume huyo hadi katika chumba kimoja cha hospitali
hiyo na kuanza kumshambulia kabla ya kumuacha akiwa hali mahututi ambapo
baadaye alifariki.
Baadhi ya
madaktari walimshambulia mwanamume huyo katika sehemu zake za siri na
kumkatakata kwa wembe kitendo ambacho kimewashtua wengi.