skip to main |
skip to sidebar
SIMU YAMWOKOA MTOTO WA MAIAKA 4 ALIYEIBWA JIJINI DAR ES SALAAM, HII NDIYO MBINU ILIYOTUMIKA KUMKAMATA MWIZI KATIKA JIJI LA TANGA.
Mama mzazi wa Marylin Repyson (kulia), Elida Fundi, akiwa amembeba
mwanawe huku akiomba jana baada ya kuwasili nyumbani kwake Changanyikeni
jijini Dar es Salaam. Picha na Fidelis Felix.
HATIMAYE kinara wa wizi wa watoto jijini Dar es Salaam, Amir Juma, amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa mkoani Tanga.
Juma anadaiwa kumuiba mtoto, Merlin Repyson (4) katika eneo la Changanyikeni siku nane
zilizopita.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,
Constantine Massawe, alikiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo akiwa wilayani
Korogwe.
“Ni kweli mtuhumiwa huyo amekamatwa huko Korogwe na polisi wetu kwa
kushirikiana na wenzao waliotoka Dar es Salaam,” alisema Kamanda
Massawe.
Alisema tayari mtuhumiwa alisafirishwa jana asubuhi kupelekwa Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
MAMA ASIMULIA
Mama mzazi wa Merlin, Elida Fundi katika mahojiano maalumu na MTANZANIA
alianza kwa kusema: “Mungu ni mkubwa nashukuru kwa maombi yenu, Merlin
alipotea siku nane zilizopita lakini amepatikana akiwa mzima.
“Ni jambo la kumshukuru Mungu, watoto wengine wakipotea wanakutwa
wametobolewa macho, lakini kwa uwezo wa Mungu na maombi yenu mwanangu
amepatikana mzima,” alisema Elida.
Alisema mwanaye alipatikana juzi saa 9:30 alasiri na kupigiwa simu na
polisi wa kituo cha Oysterbay wakitaka aende Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Alisema baada ya kufika Hospitali ya Mnazi Mmoja, alikutana na askari
polisi aliyekuwa amevaa nguo za kiraia huku akiwa amembeba Merlin ambaye
alikuwa anafanyiwa vipimo kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.
Alisema baada ya kukamilika kwa vipimo vyote, majibu yalipotoka yalionyesha Merlin hana tatizo lolote linalomsumbua.
“Pamoja na kumuona mwanangu akiwa hana ugonjwa wowote, nilishtuka mno
kwa sababu alikuwa amelegea kama vile alikuwa na njaa kali,” alisema
Elida.
Alisema baada ya kukabidhiwa mtoto wake, aliamua kumbadilisha nguo
alizokuwa amevaa kwani siku alipoibwa alikuwa na nguo tofauti na hizo.
“Baada ya kumbadilisha zile nguo niliamua kuzichoma moto pale pale
hospitali, nikiamini hazifai kuvaliwa na mwanangu… kama unakumbuka
mwanangu aliibwa Julai 15, mwaka huu mpaka nakabidhiwa jana (juzi) Julai
23,” alisema.
MTANZANIA lilifika nyumbani kwa Elida katika eneo la Changanyikeni juzi
saa 11:30 jioni baada ya kupata taarifa za tukio hilo na kushuhudia
ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wamekusanyika.
Ilipofika saa 3:30 usiku msafara wa magari mawili madogo ulionekana
ukiingia ndani ya uzio wa nyumba ya mama Merlin, huku shangwe vigelegele
vikitawala kwa ndugu na jamaa waliokuwepo nyumbani hapo.
Baada ya muda mfupi, alishuka mama Merlin akiwa na mwanaye ambaye alionekana kuwa katika hali ya kawaida.
Tukio hilo lilipokelewa kwa vigelegele, nderemo na nyimbo za kuabudu zikitawala.
Baada ya kushuka kwenye gari Merlin ndugu na jamaa walimzunguka huku
kila mmoja akiwa na shauku kubwa ya kutaka kumbeba na kupiga naye picha.
Baada ya shamra shamra hizo, Elida alishika kitabu cha sala za novena na
kuanza kufanya maombi na kuimba nyimbo za mapambio wakishirikiana na
wana ndugu.
Baada ya sala ya awali, alifika Mwinjilisti wa Kanisa Katoliki Ubungo,
Michael Kobelo na kuanza kusali tena kwa mara ya pili huku akimshika
Merlin kichwani na kumuombea.
Akizungumza na gazeti hili baada ya kumalizika shughuli zote, Elida
alisema kwa siku nane za kupotea mwanaye aliishi katika maisha magumu.
“Nimeishi katika wakati mgumu mno, sijawahi kupotelewa na mwanangu kiasi
hiki…tumesali na kufunga siku zote nane ili Merlin apatikane akiwa
katika afya njema.
“Hali ilikuwa mbaya nilisimamisha shughuli zangu zote hakuna aliyekuwa
anakula chakula, familia nzima kwa kushirikiana na waumini wenzangu
tulifunga novena ya siku tisa na leo (juzi) ni siku ya tano, tutaendelea
mpaka zitakapoisha kwa sasa tutakuwa tunamuombea afya na kumuepusha
mambo yote mabaya ambayo yataweza kumtokea baada ya hili,” alisema
Elida.
Alisema familia kwa kushirikiana na waumini wa Kanisa Katoliki
Changanyikeni, walikuwa na utaratibu wa kusali novena kila siku kuanzia
saa 2:30 usiku.
Akisimulia kupatikana kwa mtoto wake, anasema: “Nilipigiwa simu na mume
wangu ambaye naye alipigiwa na polisi kuwa mtoto amepatikana katika eneo
la Tandale kwa Mtogole,” alisema Elida.
“Nilifurahi sana nilivyomuona mwanangu lakini alikuwa amechoka mno, kitu
kingine nilichokikuta tofauti ni nywele, alikuwa na nywele fupi lakini
sio hizi wamempunguza tena tofauti na ilivyokuwa mwanzo, nilimuuliza
ulikuwa wapi akanijibu kuwa alikuwa kwa bibi,” alisema Elida.
Kuhusu Juma ambaye anadaiwa kumuiba mtoto huyo, Elida alisema aliwahi
kufanya kazi katika moja ya biashara za mume wake zilizopo eneo la
Mwenge.
Alisema Juma alimchukua Merlin na kumpeleka kwa mama aliyekuwa akiishi
na mtoto huyo siku zote mpaka polisi walipofanikiwa kumuona.
“Mimi nimeshangaa sana, hivi watu wanaishi dunia gani nasikia uko
Tandale muda wote aliokuwepo alikuwa anatoka nje na anacheza na watoto
wenzie kama kawaida,” alisema Elida.
Elida alilimwagia sifa MTANZANIA kwa kuandika ukweli wa taarifa hiyo uliosaidia kupatikana kwa mwanaye.
Merlin azungumza
Merlin alipoulizwa na MTANZANIA alikuwa wapi alijibu hivi:
“Nilikuwa nakaa na bibi mbali, nilikuwa nakula chipsi na juisi wakati nipo kwa bibi,” alisema Merlin.
MTUHUMIWA
Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, zinasema mawasiliano ya simu ndiyo yaliyosaidia alipo mtuhumiwa.
Taarifa hizo zinasema siku ya tukio mawasiliano yalionyesha Juma alikuwa eneo la Changanyikeni na baadaye Tandale kwa Mtogole.
Baada ya hapo mawasiliano yalionyesha Juma alikuwa Manzese kabla ya kupiga simu ambayo ilionyesha yuko Magomeni.
Baada ya kutoka Magomeni, alielekea Mbagala na baadaye Tandika kabla ya
kuanza safari ya kwenda Korogwe mkoani Tanga ambako alikamatwa.
MAJIRANI TANDALE
Baadhi ya majirani waliokuwa wanaishi na mama Mwanahamisi aliyekuwa
akiishi na Merlin nyumbani kwake Tandale Kwamtogole, wamesema hawakuwa
na taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo.
Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake, mmoja wa
wanafamilia ambaye ni mtoto wa dada wa mtuhumiwa alisema kipindi chote
tangu Merlin alipopelekwa hawakuwa na taarifa yoyote kama ameibwa.
“Kwa kweli huyo mtoto tangu alipoletwa na Juma zimepita kama siku tano
hivi na huyo kijana aliomba aishi hapa na sisi na baada ya siku tatu
atakuja kumchukua ampeleke kwao Tanga.
“Alituambia Merlin ni mwanaye ambaye alimzaa nje ya ndoa, hivyo endapo
angempeleka nyumbani kwake angeweza kusababisha ugomvi mkubwa na mkewe.
“Juma alikuwa anakuja mara moja moja wakati wa usiku kumjulia hali
Merlin akiwa na mfuko wa chips, jambo ambalo lilisababisha tuamini ni
mwanaye,” alisema.
Alisema siku ya tukio Amir alifika nyumbani kwao jioni akiwa na mtoto huyo na kumkabidhi kwa mama yao mdogo.
Alifafanua kuwa muda wote ambao Merlin alikuwapo nyumbani hapo, alikuwa mchangamfu kwa watu na watoto wenzake.
Alieleza Merlin alikuwa tofauti kimuonekano na watoto wengine wa mtaani
hapo kwa kuwa yeye anaonekana kalelewa katika familia ya kifahari.
“Alikuwa tofauti sana na wenzake wakiwa wanacheza utaona kabisa yeye
ametokea katika familia ya watu wanaojiweza, wakati mwingine katika
maongezi na watoto wenzake alikuwa akisema kuwa anasoma Don Bosco,”
alisema dada huyo.
MWENYEKITI
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtogole, Ramadhani Kabanga,
alisema baada ya kupokea taarifa hizo jana jioni, alifanya uchunguzi na
kubaini kuwa Juma alikuwa akiishi eneo hilo.
Alisema taarifa alizokuwa nazo ni kwamba, Juma aliamua kumuiba Merlin
kwa sababu wazazi wa mtoto huyo walimdhulumu fedha zake wakati
akiwafanyia kazi.
“Sijapata taarifa kamili kuwa ni kiasi gani cha fedha ambacho alikuwa
anadai huyo kijana hadi ikafikia hatua ya kuamua kumchukua mtoto
kinyemela wakati akijua ni kosa,” alisema.