Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma David Misime - SACP Na: Sylvester
Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma Gari lenye namba IT 7945 aina ya Toyota
Nadia ikiendeshwa na EDSON S/O MWAKABUNGU, Mnyakyusa, Miaka 31 mkazi wa
Tabata – Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na kusababisha
majeruhi kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari lingine
linalosadikiwa kuwa ni Fuso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
DAVID MISIME – SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 majira
ya saa 03:00 alfajiri katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la
Ranch ya NARCO Wilaya ya Kongwa.
Kamanda MISIME amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni EDSON
s/o MWAKABUNGU ambaye analalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu
yote, BAHATI D/O BUKUKU, Miaka 40, Mnyakyusa, Msanii wa nyimbo za Injili
na mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu
mbalimbali za mwili wake na FRANK S/O CHRISTOPHER, Muha, Miaka 20,
Msanii wa muziki wa Injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam yeye ana
michubuko usoni na mkono wa kulia.
Wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali
zao zinaendelea vizuri. Aidha Kamanda MISIME ameongeza kwa kusema kuwa
watu walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC
– Kongo, BAHATI d/o BUKUKU na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda
Kahama kwenye tamasha la Injili. Uchunguzi wa ajali hii unaendelea
ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.