Pichani
ni sehemu ya nyumba iliyoteketezwa na moto na wananchi wenye hasira
kali wa kijiji cha Lugongoni “A” Kata na Tarafa ya Nguruka wilayani
Uvinza mkoani Kigoma kwa kile kinachodaiwa ni imani za kishirikina.
Familia
nne za wakazi wa Kijiji cha Lugongoni “A” Kata na Tarafa ya Nguruka
Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma, hazina makazi baada ya nyumba zao
kuchomwa moto na nyingine kubomolewa na kundi la wananchi wa kijiji
hicho kutokana na imani za kishirikina.