Nguruwe huyu mdogo hakuwa na nia kabisa ya kufika sokoni kwa ajili ya
kuuzwa na kuchinjwa na badala yake akaamua kutumia mbinu mbadala
kutoroka kutoka kwenye gari iliyokuwa inatembea.
Nguruwe huyo alikamatwa na kamera akifanya mbinu na hatimaye kufanikiwa kutoroka kutoka kwenye Lori kuepuka kuchinjwa.
Kama ukiangalia Video hapo chini utaona alianza kwa kutoa kichwa nje na baadae kuruka mwili wote. Unaweza kuona ni kitendo cha ajabu na cha kufurahisha lakini mwisho wa siku Nguruwe huyo alijinasua kutoka kwenye mikono na watu waliokuwa wamebeba idadi kubwa ya Nguruwe kuwapeleka sokoni kuuzwa.