WAGONJWA wa kisukari wilayani
Siha mkoani Kilimanjaro, wanalazimika kutembea umbali wa kilometa 20,kutafuta
matibabu kutokana na huduma hiyo kutolewa katika hospitali ya wilaya pekee.
Kufuatia hali hiyo, wameiomba
serikali ya wilaya hiyo kuwasogezea huduma za afya katika maeneo yao.
Matibabu kwa wagonjwa wa
kisukari inatolewa hospitali moja tu ya wilaya jambo ambalo limekuwa
likisababisha wagonjwa kutembea umbali mrefu.
Katibu wa klabu ya wagonjwa wa
kisukari wilayani hapa (DIABETIC), Halima Hamisi, alitoa ombi hilo katika
hospitali ya wilaya ya Siha wakati akizungumza na umoja wa wanawake wa CCM.
Akizungumza na wagonjwa hao, Katibu
wa UWT, wilayani hapa, Zeydani Mwamba, aliishukuru serikali kwa kuimarisha miundombinu
katika hospitali hiyo ambayo imeanza kutoa huduma huku akiwataka wagonjwa hao
kuwa na subira juu ya tatizo hilo.