skip to main
|
skip to sidebar
global
Pages
Home
Thursday, May 29, 2014
HABARI: WANAFUNZI WAWILI WAUAWA KWENYE UVAMIZI VYUO VIKUU
Matukio matatu ya uvamizi katika makazi ya wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya mwaka jana na mwaka juzi, yamesababisha vifo vya wanafunzi wawili nchini.
Aidha, katika matukio hayo, mali mbalimbali kama vile simu, kompyuta mpakato na nguo, viliibwa.
Kutokana na matukio hayo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imeagiza uongozi wa vyuo vya elimu ya juu nchini, kutumia askari polisi wasaidizi au kuanzisha vituo vya askari kwenye maeneo ya makazi ya wanafunzi na vyuo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima alisema hayo bungeni jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage (CCM) aliyetaka kufahamu mpango wa serikali kuhakikisha maeneo yote ya vyuo vikuu, yanapewa ulinzi wa uhakika baada ya kujitokeza hali ya uvamizi katika makazi na maeneo ya vyuo vikuu.
Pia, mbunge huyo alitaka kufahamu idadi ya wanafunzi walioshambuliwa na mali zilizoharibiwa kutoka kwa wanafunzi hao.
Naibu waziri alisema ulinzi na usalama wa raia, wakiwemo wanafunzi wa shule na vyuo vikuu ni muhimu kwa mustakabali wa elimu ya vijana nchini. Alisema ni jukumu la wote, kama sehemu ya wajibu wa kikatiba na kijamii.
Alisema jeshi la polisi ndicho chombo chenye dhamana ya kusimamia wajibu huo, litaendelea kuchukua hatua za kupambana na vitendo vya uvamizi na uharibifu mwingine, unaotokea katika vyuo hivyo nchini hususan vya elimu ya juu.
Alisema wanaendelea kushirikiana na mamlaka, hususan uongozi wa vyuo, halmashauri, miji na serikali za mitaa kuweka miundombinu ya ulinzi shirikishi utakaosaidia kukabili matukio ya uhalifu.
“Aidha, napenda kuwaasa wanafunzi wa vyuo kutojihusisha na shughuli na mazingira hatarishi kwa usalama wao na mali zao,” alisema.
Katika swali lake la nyongeza, Mwijage alitaka kufahamu ni mikakati gani ya serikali kuweka vifaa vya usalama katika shule ili kukabiliana na uvamizi katika vyuo hivyo.
Akijibu swali hilo, Silima alisema ulinzi hasa wakati huu wa matishio ya vitendo vya kigaidi ni muhimu katika vyuo vya elimu na sehemu nyingine zenye mikusanyiko katika maeneo muhimu, kama vile hoteli.
Aidha, alisema ni vyema kuweka utaratibu wa kupekua kila anayeingia kuepuka kuingia mtu atakayesababisha madhara.
Newer Post
Older Post
Home
Popular Posts
PIGO KUBWA COLOMBIA, FALCAO KUIKOSA `MBILINGE MBILINGE` YA KOMBE LA DUNIA BRAZIL
MASHABIKI wa Colombia wamepagawa na taarifa kwamba nyota wao Radamel Falcao atazikosa fainali za kombe la dunia za mwaka huu nchini Br...
MUIGIZAJI AJIKATA UUME AKITAKA KUWA MWANAUME
Msanii Mrusi, Evgniv Sapaev, aliyecheza katika filamu mashuhuri ya ‘Burnt by the Sun 2′, alipoteza uume wake baada ya kuji...
MAANDAMANO BAWACHA: POLISI WAVAMIA OFISI ZA CHADEMA KINONDONI, HALI SI SHWARI
MAANDAMANO BAWACHA: Polisi wakiwa kwenye magari madogo 5, gari 1 la maji ya kuwasha wafika na kuzingira Ofisi za Chadema-Bawacha K...
CHADEMA YAIBUKA KIDEDEA KESI YAO MAHAKAMA YA NJOMBE DHIDI YA MBUNGE WA CCM
MAHAKAMA ya Wilaya ya Njombe imetupia mbali kesi iliyokuwa ikiwakabili viongozi wa CHADEMA mkoani hapa, ya kutishia kummwagia tindik...
UPENDO KWA MAMA NI NOVEMBER 02 SHEKH AMR ABED; SI YA KUKOSA…
KUWA WA KWANZA KUTAZAMA MDOGOMDOGO-VIDEO KUTOKA KWA DIAMOND PLATNUMZ (TESER)HAPA
Kwa Maranyingine tena mkali wa Bongo fleva hapa Bongo siku ya kesho anaachia Video zake zote mbili Mdogomdogo na kichupa alichofanya n...
BREAKING NEWS: MKE WA ALLY CHOKI AFARIKI DUNIA
MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo, Ali Choki amepata pigo la kuondokewa na mke wake, Shuea Hamis ‘Mama Shuu’ baada ya kuugua kwa m...
Samaki Mkubwa Mwenye Kupumua Kama Binadamu Aangamizwa Amazon
Samaki mkubwa zaidi wa maji matamu Arapaima Samaki aliye na urefu wa mita tatu aliyekuwa maarufu katika mto Amazon amevuliwa ...
MKUNDI NI SHIIDAH YAANDAA TAMASHA BURE LAKINI PIA KUWAPELEKEA WAKAZI WA MOSHI BURUDANI YA INJILI.
Tamasha la Upendo kwa mama litafanyika tena kwa mara ya pili ndani ya jiji la Arusha kutokana na kuvunjika kwa tamasha la awali kutokana na ...
KINANA : VIONGOZI WA KIJIJI WAACHE KUUZA ARDHI BILA KUWASHIRIKISHA WANANCHI
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na wamasai katika kijiji cha Ayamango (Gallapo) ambapo alikuwa na kazi ya kufu...
[URL=http://info.flagcounter.com/UhIW][IMG]http://s03.flagcounter.com/count/UhIW/bg_FFFFFF/txt_000000/border_CCCCCC/columns_2/maxflags_12/viewers_0/labels_0/pageviews_0/flags_0/[/IMG][/URL]
flags.es
www.playonlineroulettex.com
The following text will not be seen after you upload your website, please keep it in order to retain your counter functionality
silver lotto system review
Live Traffic Stats
Ads 468x60px
Followers
PGA Head Teaching Professional
Unknown
View my complete profile
Powered by
Blogger
.