global

global

Pages

Thursday, May 29, 2014

WATOTO WATATU WAFUNGIWA NDANI MWEZI MMOJA KWA HOFU YA KUBAKWA

Sambamba na hayo mama huyo ameiomba serikali kumsaidia kutokana na adha kubwa aliyonayo ya kubakwa kwa watoto wake huku mtuhumiwa wa kesi hiyo ya ubakaji akiwa ameachiwa huru baada ya kuwa kizuizini takribani miezi sita tu.

Kwa upande wao wananchi waliojitokeza kwenye adha hiyo ambayo ilihudhuriwa na viongozi wa kijiji, wamekiri kufungiwa ndani kwa watoto hao ambao walikuwa  kwenye chumba chenye uchafu uliokithiri.

Sambamba na hayo wanakijiji hao wamesema kuwa mama huyo anajihusisha na mambo ya kishirikina, kwani ameanza muda mrefu kuwafungia watoto hao japo wakati Juma akiwa ameshikiliwa na jeshi la polisi watoto hao waliendelea kubakwa ndani kwao huku milango yote ikiwa imefungwa na kufuli.

Rajabu Michael Kigwamke ambaye ni baba wa mtoto huyo aliyewahi kubakwa alikanusha kutomhudumia mtoto huyo na kudai kuwa amekuwa akishirikiana na mke wake huyo katika baadhi ya huduma ikiwa ni elimu pamoja na mavazi.

Kigwamke amesema kuwa baada ya kupata taarifa ya kubakwa na kulawitiwa kwa watoto hao aliamua kumkamata Juma Msungu mtuhumiwa wa tukio hilo ila ajabu ni pale ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa kizuizini, lakini bado watoto hao waliendelea kubakwa. 
Aidha akitoa taarifa hiyo Afisa Mtendaji wa kijiji cha Tanangozi Bi Lucy Msigwa alisema kuwa tarehe 26 mwezi huu wa tano alipigiwa simu na mgambo wa kijiji Bw Rajabu Michael Kigwamke kwamba kuna watoto wamefungiwa ndani ya nyumba yake na  baada ya kufika katika eneo la tukio aliwakuta watoto hao wakiwa wamefungiwa ndani huku wakiwa uchi wa mnyama, watoto hao walikuwa watatu, wawili ni mapacha wana umri wa miaka 2 na Yule ambaye ni mkubwa ana miaka 5.Afisa mtendaji alimuamuru balozi kuufungua ule mlango na kuwachukua watoto hao kwenda nao hadi ofisi za serikali ya kijiji hadi pale alipofika mama huyo na kukiri kuwafungia watoto hao kutokana na kuogopa watoto wake kuendelea kubakwa hivyo aliamua kumkabidhi mtoto mmoja wa kiume kwa baba yake.