Saturday, October 4, 2014
Tuesday, September 2, 2014
RAIS KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA AMANI NA USALAMA WA BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA JIJNI NAIROBI
SHETANI KAWEKEZA KWENYE KILA KITU KIZURI
Kila kwenye kitu kizuri, shetani kaweka mguu wake.
(Nazungumzia maadili ya vijana). simu ni moja ya kitu kizuri, lakini shetani kaweka mguu wake kuharibu maadili ya vijana.
Nilijaribu kujiuliza kuwa kwanini hata sukari na nyama watu wanakatazwa na kuruhusiwa kula matembele? why?
Kila kitu kizuri, shetani amewekeza na kujipachika
(Nazungumzia maadili ya vijana). simu ni moja ya kitu kizuri, lakini shetani kaweka mguu wake kuharibu maadili ya vijana.
Nilijaribu kujiuliza kuwa kwanini hata sukari na nyama watu wanakatazwa na kuruhusiwa kula matembele? why?
Kila kitu kizuri, shetani amewekeza na kujipachika
Monday, August 18, 2014
UTABIRI WA ASKOFU KAKOBE UNAENDELEA KUTIMIA, IKULU NA MWANASHERIA WA SERIKALI WATOFAUTIANA
Ni mazingaombwe yanayoweza kupatikana tanzania pekee duniani.
‘ikulu inatoa tamko lao kuwa bunge litaendelea na katiba lazima ipatikakane bila hata ya kuwepo umoja wa katiba ya wananchi [ukawa].
Samaki Mkubwa Mwenye Kupumua Kama Binadamu Aangamizwa Amazon
Samaki mkubwa zaidi wa maji matamu Arapaima
Samaki mkubwa zaidi wa maji matamu Arapaima
Samaki aliye na urefu wa mita tatu aliyekuwa maarufu katika mto Amazon amevuliwa hadi ameangamia
Watafiti wamedhihirisha kuwa samaki huyo mkubwa hapatikani tena katika maeneo aliyokuwa maarufu.
Imebainika sasa kuwa samaki wa Arapaima alipatikana katika maeneo 8
kati ya 41 zilizofanyiwa utafiti, na idadi ya samaki huyo ilikuwa ndogo
sana kulikoilivyokuwa inatarajiwa.
Wavuvi walipewa mafunzo jinsi ya kuhesabu samaki hao ili kufanikisha utafiti huo mkubwa.
Watafiti walikata kauli kuwa athari za uvuvi kwa samaki wa kitropiki zilikuwa mbaya zaidi ya ilivyoaminika hapo awali.
Matokeo ya utafitihuo yaliripotiwa kwa shirika la uhifadhi wa mazingira
yanayozalisha viumbe vya majini ''Aquatic Conservation: Freshwater and
Marine Ecosystems''.
Arapaima huweza kuwa na uzani wa kilo 181 na ni mojawapo ya samaki wakubwa zaidi wanoishi katika maji yasiyo na chumvi.
Samaki hao hupumua hewa sawa na binadamu, hivyo basi huibuka kutoka
majini kupumua kila baada ya dakika kati ya 10-15 hivyo basi huwa ni
rahisi kuwakamata.
Ukubwa wa Arapaima huvutia wavuvi kuwawinda na aghalabu huwanasa kwa kutumia chusa au nyavu za uvuvi.
Karne moja iliyopita, idadi ya Arapaima ilikuwa kubwa katika mto wa
Amazon, lakini watafiti wanasema kuvua kupita kiasi kumesababisha idadi
hiyo kupungua kwa kiwango kikubwa sana.
Hapo awali, utafiti nadharia ulitabiri kuwa uvuvi hauwezi kuangamiza
aina fulani ya samaki majini kwani wavuvi huenda kuvua maeneo tofauti
idadi ya samaki inapopungua katika eneo moja.
Wanasayansi, wakiongozwa na Leandro Castello, kutoka Virginia Marekani,
walitaka kufahamu afya ya samaki wa Arapaima walioko eneo la chini la
Amazon.
Aidha walitaka kugundua iwapo shughuli za uvuvi ziliunga mkono au kupinga utabiri wa nadharia tofauti.
Kuna nadharia zinazopendekeza kuwa samaki wakubwa, walio ghali, na
ambao ni rahisi kukamatwa huweza kuvuliwa na kuisha majini, huku
nadharia zingine zikipinga msimamo huo.
Watafiti hao walihoji wavuvi 182, walioaminika kuwa magwiji na wenzao,
katika jamiii 81, zinazoishi katika eneo la kilomita 1,040, la Amazon.
Shughuli hiyo ilijumuishwa hesabu ya Kulifanywa ya samaki katika jamii 41 kati ya jamii zilizohojiwa.
Wavuvi nane walifunzwa kuhesabu idadi ya Arapaima pindi tu walipotokea majini.
Matokeo ya hesabu hiyo ni kuwa idadi ya Arapaima ilikuwa imepunguka
katika asilimia 57% ya eneo la utafiti, Arapaima hawakuwepo katika
asilimia 19% ya eneo hilo, na walivuliwa kupita kiasi katika asilimia
17% ya eneo hla utafiti, huku asilimia 5% tu wakifanya uvuvi
unaokubalika. Kwa 2% ya jamii zilizofanyiwa utafiti, samaki hao
hawakuvuliwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)


